Wapendwa washirika na waomba ruzuku.
Uongozi wa Mfuko, unapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu majibu ya maombi ya ruzuku ya miradi inayolenga kukuza uelewa wa haki za wanawake katika kipindi hiki cha kupambana na Corona (Covid19). Awali majibu yalikuwa yatoke tarehe 14 Mei 2020 kama ilivyoelezwa kwenye tangazo, kutokana na kupokea maombi mengi kuliko ilivyotarajiwa, hivyo kupelekea taratibu za kuchakata na kuchagua mashirika na vikundi kuchukua muda zaidi.
1 Juni 2020, Mfuko utatoa majibu kwa wale waliopata na kuchaguliwa, ikiwa hukupata taarifa ya kuchaguliwa ifahamike kwamba shirika lako au kikundi chako hakikufanikiwa kuchaguliwa katika awamu hii ya miradi ya Corona (Covid 19).
Tunatanguliza shukrani za dhati kwa uvumilivu na uelewa.
Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji,
Mary Rusimbi
WFT-Trust,
Dar es Salaam
20 Mei 2020