Wapendwa washirika na waomba ruzuku.
Awali ya yote tunapenda kuwashukuru wote mliowasilisha maombi ya ruzuku kwetu kwa mwaka 2020.Tunafurahishwa na idadi ya waombaji wa ruzuku inayoendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.
Pili tungependa kuwajulisha kuwa WFT-Trust kama taasisi imekuwa sehemu ya kuathirika na kubainika kwa wagonjwa wa mafua makali ya CORONA kama ambavyo tumetaarifiwa na mamlaka husika tangu juzi.
Hali hii ya kuwepo kwa wagonjwa hawa nchini mwetu imetulazimisha kupitia taratibu zetu za kiusalama wa afya na taratibu zetu za utoaji huduma.
Sisi kama taasisi tumefanya tafakari ya kina kuhusu athari mtambuka za hali ya ugonjwa huu na jinsi ambavyo tunapaswa kuchukua tahadhari ili kuepusha maambukizi mapya ya ugonjwa wa CORONA kwetu sisi wenyewe lakini pia kwa wadau na washirika wetu mbalimbali maana kama tujuavyo ‘’Kinga ni Bora Kuliko Tiba”. Baada ya tafakuri ya kina tumefanya maamuzi yafuatayo ambayo yamepelekea kuwepo na mvurugizo wa taratibu zetu za kawaida za utendaji kazi na hususan utaratibu wa utoaji ruzuku.
Hatua tulizochukua:
Athari za hatua hizi:
Hitimisho:
Pamoja na nia yetu njema ya kuharakisha michakato ya kutoa ruzuku kwa washirika wetu tunatambua changamoto mbalimbali zinazotokana na hali ya ugonjwa huu hatari na wajibu wetu wa kujali na kulinda afya na usalama wa wafanyakazi wetu,washirika wetu pamoja na wadau wetu mbalimbali.
Moja ya adhari kubwa ya hatua hizi ni kuchelewa kwa mchakato wa utoaji wa ruzuku kwa mwaka huu ambayo itaathiri pia uwezo wa wadau wetu katika kutekeleza afua mbalimbali za utetezi wa haki za binadamu na hususan hati za Wanawake,Wasichana na Watoto.
Hivyo kwa taarifa hii tunaomba mpokee salamu zetu za upendo na mshikamano kwenu nyote katika kipindi hiki kigumu.
Mwisho tunakisia kuwa michakato kwa ujumla itachelewa kwa muda wa kati ya wiki 4 mpaka 6.
Tunaomba radhi kwa uchelewesho huu na tunawaomba msikate tamaa na kwamba mara tu baada ya hali ya udhibiti wa mlipuko wa ugonjwa huu kutengemaa tutaendelea na mchakato wa utoaji wa ruzuku kama kawaida.
Tutaendelea kupatikana na kutoa huduma na au ushauri mbalimbali kwa wadau wetu kupitia mawasilano ya simu kwa nambari 0753 912130, barua pepe kwa anuani ya info@wft.or.tz na inapowezekana kupitia mikutano mkondoni (Online meetings).
Asanteni Sana
Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji,
Mary Rusimbi
WFT-Trust,
Dar es Salaam
23/03/2020.