TANGAZO LA KUTUMA MAOMBI YA RUZUKU YA MIRADI MIDOGO MIDOGO MWAKA 2018.

MIRADI INAYOSHUGHULIKIA MASUALA MBALI MBALI YA UTETEZI WA HAKI ZA WANAWAKE NA WASICHANA. | Mwisho wa kupokea maombi ni 28 Februari 2018

Shirika la Women Fund Tanzania (WFT) lilianzishwa mwaka 2008 likiwa na lengo la kutoa mchango wake katika kuwawezesha wanawake na vijana wa kike na hasa wale walio pembezoni mwa jamii zao kujijengea uwezo na sauti zaidi kwa kufikiwa na maarifa, ruzuku na kwa kuimarisha mikakati yao ya ujenzi wa nguvu za pamoja katika ngazi mbali mbali, na haswa kwenye ngazi za jamii.

Kwa Mwaka 2018, WFT inakaribisha maombi ya ruzuku ya miradi midogo ya utetezi wa haki za wanawake na vijana wa kike iliyo na gharama kati ya Tsh 6,000,000.00 mpaka Tsh 10,000,000.00 na maeneo yatakayopewa kipau mbele ni pamoja na:

 • Upingaji wa ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake na vijana wa kike hasa upingaji wa maswala ya rushwa ya rushwa ya ngono.
 • Kukuza haki za kiuchumi za wanawake ikijumuisha haki zao za kushiriki na kunufaika katika sekta ya madini, gasi na mafuta.
 • Kukuza sauti za wanawake katika mapambano ya mabadiliko ya tabia nchi, ardhi na maji.
 • Kukuza mitandao na juhudi mbali mbali zinazolenga katika kuunganisha nguvu za wanawake ili kuimarisha harakati zao nchini ikilenga haki za makundi yaliyopo pembezoni kama (wanawake wanoishi na ukimwi, wanawake walemavu, wazee nakadhalika).
 • Kukuza haki za wanawake na wasichana waishio katika mazingira hatarishi, wakiwemo wakimbizi.
 • Kukuza haki za wanawake na vijana wa kike za kikatiba na uongozi kwa ujumla.
 • Miradi inayokuza mikakati ya kutunza na uandishi wa kumbukumbu muhimu za mwanamke mmoja mmoja au taasisi katika kuthamini na kuonyesha nguvu na mchango wa wanawake vijana wa kike katika harakati mbali mbali za kuleta maendeleo nchini.
 • Ushiriki mpana wa jamii katika kukuza haki ya elimu ya mtoto wa kike.

Vifuatavyo ni vigezo vitakavyotumika wakati wa uchaguzi wa wazo bora la mradi:

 • Ubora wa andiko la awali kuhusu mradi linaloonyesha uhusiano wa karibu kati ya tatizo lililopo, mikakati iliyopangwa pamoja na matokeo yanayotarajiwa.
 • Uwezo wa Shirika au Kikundi katika kutekeleza mradi wanaoomba.
 • Wazo la mradi linalo akisi ushirikishwaji wa wadau wa sekta katika kupanga na kutekeleza mradi hasa kwa kushirikishwa waathirika wakubwa wa tatizo linalohitaji kushughulikiwa.
 • Kujenga ubia kati ya mashirika ya kutetea haki za wanawake yanayolenga kuimarisha mitandao inayofanya kazi ya Kukuza haki za wanawake katika ngazi mbali mbali.
 • Muendelezo, na uwezo wa kuonyesha jinsi ya kuhifadhi na kutumia mifano mizuri ya utekelezaji katika ngazi za juu zaidi.
 • Ubunifu wa andiko la awali la mradi.

Muombaji wa ruzuku atafuata hatua mbili zifuatazo:

 • Uwasilishaji wa wazo la mradi (tumia miongozo/ fomu yetu) ikielezea mapendekezo/mawazo na kuwasilishwa kabla ya tarehe 28 Februari 2018.
 • Baada ya uchambuzi kufanywa na kamati ya uchambuzi miradi, watakaochaguliwa watakaribishwa kuleta andiko kuu la mradi.

Tafadhali, tumia miongozo/fomu yetu ya wazo la mradi kama inavyopatikana kupitia tovuti yetu: www.wft.or.tz. Fomu (miongozo) pia unaweza kutumiwa Kwako kwa email pale itakapoombwa au inaweza kuchukuliwa ofisi za WFT wakati wa saa za kazi (Ukiwa na flash).

Tafadhali ambatanisha vitu Vifuatavyo katika maombi yako:

 • Cheti cha usajili wa Kikundi/Shirika
 • Katiba ya Kikundi/ Shirika
 • Picha za ofisi za Kikundi/Shirika
 • Barua ya bank kuthibitisha uhai wa account/bank statement

Mwisho wa kupokea maombi ni 28 Februari 2018

 • Kwa kupitia email, grants@wft.or.tz
 • Au WFT, S.L.P 79235, Dar es salaam
 • Au kuleta ofisini kwetu, Nyumba namba 659 mtaa wa Mikoroshini (Msasani) Dar es Salaam.

Kwa maelezo zaidi unaweza kutupigia 0753 912 130

WATAKAO JULISHWA NI WALE TU WALIOCHAGULIWA, IFIKAPO TAREHE 15 MARCH 2018, HUJAJULISHWA BASI ANDIKO LAKO HALIKUCHAGULIWA.

FUNDING OPPORTUNITY ANNOUNCEMENT FOR SMALL-SCALE PROJECTS.

PROJECTS SHOULD FOCUS ON EMPOWERMENT AND STRENGTHENING WOMEN’S AND GIRLS’ RIGHTS MOVEMENT IN THE COUNTRY. | Application deadline: 28th February 2018

Women Fund Tanzania (WFT) is a Women Rights Fund registered in September 2008. Its vision is to see a Tanzanian Society where women realize their full potential and engage in transformation for empowerment, and social justice. As movement builders, and as an activist and feminist organization, WFT’s overall goal is to contribute towards women’s rights and empowerment, and to women’s movement building through implementing a functional funding mechanism for women in the country. The Fund does this through making grants, strengthening women’s and institutional capacity on women’s rights issues, building strategic alliances and mobilizing resources.

In 2018, WFT will be accepting small grants applications for project funds between Tsh 6,000,000.00 to Tsh 10,000,000/= for interventions addressing the following thematical areas which goes:

 • Violence against women and young girls with a particular focus on addressing sexual corruption/sextortion issues.
 • Economic rights of women including promotion of women’s and girl’s rights in the extractive industries, mining, gas, oil.
 • Environmental justice rights for women and young girls projects for promoting voices of women and girls in addressing issues of climate change, land grabbing, land rights and water rights issues.
 • Networking and coalition building interventions to strengthen the women’s movement (s) in Tanzania with a particular focus on inclusion young women and minority groups (women living with disabilities, HIV-AIDS, elderly women, etc.) in sectorial or broader women’s rights movement.
 • Political and leadership rights of women with a particular focus on promoting young women issues into leadership.
 • Projects promoting documenting her-stories/telling stories of women’s struggles/at individual and institutional level next to advocating for broader women and girls visibility through innovative approaches, intervention, especially in rural areas.
 • Innovative projects on empowering and participatory community engagement approaches for enhancing girl’s educational rights.
 • Innovative projects on empowering and participatory community engagement approaches for enhancing women and girls migrants’ rights.

The following selection criteria will be taken into account:

 • Quality of the submitted Concept Note, ensuring that there is a strong link between the problem to be addressed and the strategies and measurable results anticipated.
 • Relevant Institutional capacity to implement the proposed project.
 • The Concept Note should reflect a multi-stakeholder participation in formulation and implementation, including those most affected by the situation to be addressed.
 • The Concept Note should reflect efforts towards building partnerships between women’s rights organisations at different levels with the purpose of forming/strengthening functional networks and coalitions for promoting women’s rights and empowerment.
 • Sustainability, replicability and potential to demonstrate and document models that can be taken to larger scale.
 • Innovativeness of the proposed project/activities.

Requirements:

Application for these Grants will follow a two-stage process:

 • Submission of a Concept Note (5 pages max) describing the proposed idea/initiative to be implemented. Send your complete Concept Note before 28th February 2018
 • Review/selection by WFT’s Selection Committee where after selected applicants will be invited to submit a full project proposal.

Use our Concept Note format as published on WFT’s website: www.wft.or.tz. The Concept Note format can also be sent to you by e-mail upon request or it can be picked up from WFT’s office during office hours (Come with a flash drive)

Concept note submitted should have the following attachments:

 • Copy of registration
 • Organizational constitution
 • Office Picture
 • Letter from the bank or bank statement to verify if the account is active

You can Please, send your complete Concept Note before 28 February 2018 to, by

 • Email to: grants@wft.or.tz
 • Through :WFT, P.O.Box 79235, Dar es Salaam by mail
 • Hand to: or WFT, 659 Mikoroshini Street (Msasani), Dar es Salaam by hand

For any queries contact us on Tel WFT: 0753 912 130

Please Note the Following:
 • Only complete Concept Notes will be considered; other documents will not be considered at this stage
 • Only short-listed applicants will be contacted
 • If you have not been contacted by the 15th March 2018 your application has not been considered this time

The eligible activities for WFT funded projects will be prepared by the Secretariat, and reviewed and approved by the Selection Committee, while the Board of directors is informed on the emerging trends and results. The eligible activity may vary from time to time. The procedure on how to prepare the eligible activities is narrated in a step-by-step competitive grant making procedure. To find out more Read the GRANT MAKING GUIDELINES

A CALL FOR PROPOSALS is issued and grant proposals are accepted only during scheduled application periods: we do not accept unsolicited proposals outside of this time. Requests for proposals will be posted on the site.